Friday, March 13, 2009

Martin,kijana mdogo vipaji lukuki


Ni kijana wa makamo hivi aliezaliwa miaka 21 iliopita hapa jijini Dar,hakika ni kijana ambae anaonekana kuwa na vipaji vingi (mati talented) ambavyo kwa mujibu wa mazungumzo yake leo mchana na Jiachie ati vyote ana vimudu.
Unajua vipaji gani hivyo.!? binafsi ameniambia kuwa yeye ni Mbunifu wa mavazi,mwanamitindo,muigizaji wa filamu na pia ni grafix dizaina na vyote ana vimudu kwa ufasha kabisa.
Jina lake halisi ni Martin Andrew Kadinda ambaye alianza fani ya uanamitindo mnamo mwaka 2004,aliposhiriki maonesho kadhaa ya mavazi likiwemo la Tanzania Super Model lililofanyika katika ukumbi wa Walter Front zamani Nssf ,Red Carpet,Kimasomaso,Identint pamoja na onesho la 4 u2.
Anasema pamoja na kushiriki uanamitindo, pia haikumchukua muda akajifunza masuala ya ubunifu wa mavazi mbalimbali, ikawa bahati kwake akashiriki pia mashindano kadhaa likiwemo la Swahili Fashions week lililofanyika diamond Jubilee,Red Carpet appearance lililofanyika hoteli ya Regency Park na baadaye onesho la Red in Lady lililofanyika ndani ya hotel ya Kempisk jijini Dar hivi karibuni.
Anasema kutokana na uzoefu alioupata amefanikiwa kubuni/kudizaini mavazi ya aina mbalimbali kwa watu tofauti tofauti akiwemo mtangazaji wa redio ya Clouds Fm Bibie Sofia Kessy,Aliyewahi kuwa miss Tanzania no 3 Pendo Leizer pamoja na mlimbwende mwingine kutoka miss Kinondoni Fay Antony na watu wengine ambao anakiri wazi kuwa wamevutiwa sana na kazi yake ya ubunifu.
Martin anawataja wabunifu wa ndani na nje ambao wamempa hamasa kubwa kiasi hata yeye kujiingiza kwenye fani hizo kuwa ni Farouk kutoka Zanzibar ambaye ni mbunifu wa anaejulikana kimataifa pamoja na Dorcen and Gabana ambao wao huko ughaibuni.
Akibainisha changamoto zilizomo kwenye fani hiyo ya ubunifu wa mavazi, Martin anaweka wazi kuwa Wabunifu wengi wanapenda kutengeneza/buni mavazi ya kike sio kwamba wanapenda,bali inatokana na kuwa asilimia kubwa ya wanaume bado hawajakuwa na mwamko wa kukubali ubunifu wa nyumbani (Tanzania),kwamba wengi wao wanayakacha sana mavazi yanayobuniwa na wabunifu wa Tanzania na badala yake hukimbilia mavazi ya kigeni.
"Halafu suala lingine ni kuhusu Serikali, Serikali yenyewe inatakiwa itutambue Wabunifu wa mavazi na kutupa sapoti kwa namna moja ama nyingine,ili fani hii iheshimike na ikubalike ndani ya nchi ndio ipate kutoka nje, tukifanikiwa kwa hilo naamini nasi tutafika bali, kwani angalau juhudi zitakuwa zimeonekana kutoka serikalini"anasema Martin
Akizungumzia fani yake nyingine ya ugizaji,Martin anasema kuwa mpaka sasa ameigiza filamu inayoitwa Friend of Mine ambayo tayari iko sokoni mpaka sasa,nyinginezo ni Men in Town pamoja na filamu iitwayo Ghost.

No comments:

Post a Comment